KIUNGO wa Yanga, Papy Tshishimbi, juzi Jumamosi alifanikiwa kuziba vyema pengo la kiungo wa timu hiyo, Mzimbabwe, Thaban Kamusoko katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kupiga pasi 24 pamoja na kuonyesha uwezo mkubwa katika nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Juzi Jumamosi Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa mjini Bukoba, Kagera.
Kamusoko hakusafiri na timu hiyo kutokana na kukabiliwa na majeraha ya goti kitendo kilichoongeza hofu kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kwa mchezaji atakayeweza kucheza nafasi yake kabla ya Tshishimbi kuonyesha uwezo mkubwa kwa kucheza nafasi hiyo na kusababisha kusahaulika kabisa.
Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza Tshishimbi alionekana kutawala eneo la kiungo cha juu kwa kupiga pasi tamu kwa washambuliaji, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa ambazo ni 18 zilizofika kwa walengwa.
Tshishimbi katika kipindi cha pili, alirudi kucheza kiungo cha chini na kufanikiwa kupiga pasi sita za uhakika na pasi kumi zilizopotea, huku akipiga shuti moja ambalo lilipaa juu ya lango la Kagera Sugar.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment