Messi amekuwa tishio kubwa kwa sasa ulaya. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 4 October 2017

Messi amekuwa tishio kubwa kwa sasa ulaya.

Kiwango cha mshambuliaji nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi, kiko “on fire” hasa.

Messi amecheza mechi tisa za La Liga na kufanikiwa kufunga mabao 11 lakini amefunga mabao 15 katika michuano yote ikiwa ndiyo mwanzo tu wa msimu.

Takwimu zinaonyesha msimu huu ndiyo bora zaidi kwa Messi kuanza kuliko mingle yote tokea ajiunge na FC Barcelona.

Tayari ameishacheza mechi mbalimbali za michuano kama La Liga, Super Cup ya Hispania na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mwendo huo wa Messi unamfanya kuwa ndiye mshambulizi tishio zaidi katika kipindi hiki.

Mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real madrid anaonekana kutokuwa na mwanzo mzuri.

No comments:

Post a Comment