Hatimaye Hamisa Mobetto Amuweka Wazi Baba Wa Prince Abdul. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 19 September 2017

Hatimaye Hamisa Mobetto Amuweka Wazi Baba Wa Prince Abdul.

Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka mambo hadharani kwa kumtaja baba wa toto wake wa pili AbdulLatif kuwa ni Diamond Platnumz.

Kwa mujibu wa akaunti ya mtandao wa Instagram ya mtoto huyo inaonyesha jina kamili la mtoto kuwa ni “Dully Dangote (AbdulLatif Naseeb Abdul Juma )Lion 🦁 (Leo) -8|8|2017 TanzanianBaby 👑 @hamisamobetto & Diamond Platnumz Son.”

Miezi kadhaa nyuma Diamond Platnumz alikuwa akikana kuhusika kutoka kimapenzi na mwanamitindo huyo na pia kukana mimba aliyokuwa nayo mrembo huyo.

Hamisa ambaye alianza kutaja majina ya baba wa mtoto huyo miezi kadhaa nyuma kwa herufi za mwanzo, hatimaye ameweka jina lote la baba huyo katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram.

Abdullatif ni mtoto wa pili wa mrembo huyo ambapo mtoto wa kwanza Fantasy alizaa na Mkurugenzi wa EFM, Majay.



No comments:

Post a Comment