Wastara amedai kuwa maisha yake yamebadilika... - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 4 February 2018

Wastara amedai kuwa maisha yake yamebadilika...

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amefunguka na kudai maisha yake yamebadilika tokea alipopata ajali kwa mara ya kwanza na kuwa ya kusaidiwa kwa asilimia kubwa na watu wake wa karibu pamoja na wananchi kiujumla wanaoguswa na kuugua kwake.

Wastara amebainisha hayo leo wakati alivyokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Taifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya kuanza safari yake ya kuelekea nchini India.

"Natamani kuwa na 'Foundation' yangu, kituo cha watoto yatima kwa sababu tokea nilipopata ajali maisha yangu yamekuwa yakusaidiwa tu asilimia kubwa japo ni msanii na nina jina lakini vitu vingi nimekuwa nikifanya kwa kusaidiwa kwa hiyo natamani siku moja nije nami kusaidia watu. 'I wish' na nina amini kwa nguvu ya Mungu itatokea tu", amesema Wastara.

Pamoja na hayo, Wastara ameendelea kwa kusema "nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia".

Kwa upande mwingine, Wastara amesema hata akirudi kutokea katika matibabu yake hafikilii kuacha sanaa ya filamu kutokana anafanya kazi hivyo kutoka ndani ya moyo wake.

No comments:

Post a Comment