Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Snura amesema tuhuma zinazomkabili kuhusu kijana huyu anayejulikana kwa jina la Minu Calypto, zimemfanya atoe siri ambayo hakutaka wajue, kuwa kijana huyo sio mpenzi wake bali amefanya naye video ambayo haijatoka, na ndipo zilipopigwa picha za mahaba zilisosambaa mtandaoni.
“Mimi na Minhal hatuna mahusiano, kisa picha!!? Picha ile ni video jamani hii sasa mnanilazimisha niseme siri sasa, ni video ambayo haijatoka na imechelewa kutoka kwa sababu nimeimba na Aslay, na Aslay alikuwa na project yao ya Valentine, ndio maana amechelewa kuingiza vipande vyake ndio maana imechelewa kutoka”, amesema Snura.
Kijana huyo ambaye kwa sasa ameingia kwenye muziki wa bongo fleva, anatajwa kuwahi kutoka kimapenzi na msanii wa filamu bongo, Nisha bebe.
No comments:
Post a Comment