Nikki wa pili amefunguka kuhusu Joh Makini kuja na bidhaa ya Kondomu - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 12 October 2017

Nikki wa pili amefunguka kuhusu Joh Makini kuja na bidhaa ya Kondomu

Rapper wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amezungumzia taarifa za Joh Makini kuja na bidhaa za kondomu.

Nikki ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kihasa’ amesema kuhusu ujio wa bidhaa hizo bado mazungumzo yanaendelea ila kitu ambacho kipo.

“Ile ni biashara ya Joh Makini sitaki kuizungumzia ila nachoweza kusema ni kwamba kuna watu ambao wapo, wapo katika mambo ya testing,” alisema Nikki wa pili.

“Wakifanikiwa na kukidhi vigezo vyote Joh Makini atakuja public, bidhaa zake zitakuja public lakini kwa sasa wapo kwenye meza wanafanya kazi,” ameongeza.

Iwapo dili hilo litafanikiwa Joh Makini ataungana na wasanii Bongo Flava kama Diamond, Jux, Shetta na wengineo kutangaza bidhaa zao.

No comments:

Post a Comment