SIKIA POVU LA HAJI MANARA KUWAHUSU EVERTON. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 14 July 2017

SIKIA POVU LA HAJI MANARA KUWAHUSU EVERTON.

Msemaji machachari aliyefungiwa klabu ya simba Haji Manara ametoa ya moyoni kuwa hajapendezwa na timu ya Everton inayotokea Uingereza Kuondoka Nchini bila ya kucheza na klabu ya simba na yanga.
Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kumalizika mchezo wa kirafiki kati ya Everton dhidi ya Gor Mahia ya huko kenya katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
“Sijapenda kwa club zetu mapacha kukosa nafasi ya kucheza na kina Rooney leo, ila mungu ni fundi maana wangepata nafasi wale jamaa wangejiita wa MBINGUNI jina la kimataifa wangeliacha #Everton in Tz.”
Hayo ndiyo aliyo yazungumza haji manara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao Everton waliibuka na ushindi wa goli mbili huku Gor Mahia wakiwa na goli Moja.
Kwa matukio ya picha zaidi zipo hapa chini. Pia endelea kutembelea Instagram,Facebook na Twitter @ erickpicson.

No comments:

Post a Comment