Shilole apigwa faini kisa hiki hapa.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 1 March 2018

Shilole apigwa faini kisa hiki hapa..

Mahakama ya Mwanzo wilaya ya Kinondoni imemhukumu msanii 'Shilole' kulipa TSh Milioni 14 kwa kosa la kuchukua malipo ya show kiasi cha TSh Milioni 3 kutoka kwa Mary Mussa na kushindwa kufika kwenye shoWhiyo usiku wa Pasaka mwaka 2017.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo leo Machi 1, 2018 baada ya kumkuta Shilole na hatia ya kutapeli fedha hizo, kutokana na kushindwa kufika kwenye show husika kama ambavyo walikuwa wamekubaliana na Mary Mussa jambo ambalo lilisababisha Mary kupata hasara kutokana na mashabiki kufanya vurugu kwa kutomuona Shilole kwenye show hiyo kama ambavyo walitangaziwa awali.

Mahakama hiyo pia imempa muda wa wiki moja msanii huyo kuwa awe ameshalipa fedha hizo kwani kinyume na hapo mahakama itashikilia mali za msanii huyo.

Msanii Shilole aliambatana na mumeo Uchebe mahakamani pamoja na wakili wake, ambapo baada ya hukumu hiyo msanii huyo hakutaka kuongea chochote na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment