Enock Bella ajibu tuhuma ya wasanii walio kuwa Yamoto Bend hawaelewani.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 7 March 2018

Enock Bella ajibu tuhuma ya wasanii walio kuwa Yamoto Bend hawaelewani..

Mwanamuziki Enock Bella amefunguka kuhusu tuhuma kuwa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band kwa sasa hawaelewani.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Kidogo’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa hakuna ugomvi wowote kati yao na ipo siku watu watawasikia wakishirikiana katika ngoma tofauti tofauti.

“Ukifika muda tutachukua ngoma za Yamoto Band na kupeleka watu, usishangae kusikia ngoma yangu na Aslay, pia usingae kusikia ngoma mimi na Beka, pia usishangae kusikia ngoma na Maromboso, bado upendo wetu upo pale pale,” amesema.

Hadi kufikia sasa wasanii wote waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band wametoa kazi zao binafsi, Aslay anaongoza kuwa na nyimbo nyingi zaidi na zilizofanya vizuri akifuatiwa na Beka Flavour, Enock Bella na Mbosso wamekuwa wa mwishoni kutoa ngoma zao.

No comments:

Post a Comment