TUNDU LISU APELEKWA NAIROBI KENYA KUTIBIWA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 7 September 2017

TUNDU LISU APELEKWA NAIROBI KENYA KUTIBIWA.

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma usiku huu kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Lissu ambaye alijeruhiwa akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D , mjini Dodoma baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulika.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amesema, katika safari hiyo Lissu ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Selasini amesema kuwa Lissu anapelekwa katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi. Ndege hiyo iliyombeba ya 5H-ETG imeondoka katika Uwanja wa Dodoma saa sita na robo usiku.

No comments:

Post a Comment